Mkuu wa jeshi la Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan azuru Qatar kujadili hali ya vita

  • | VOA Swahili
    205 views
    Mkuu wa kijeshi wa Sudan Jenerali Abdel Fattah al-Burhan amezuru Qatar hii kwa mazungumzo juu ya hali ya vita nchini mwake. Shirika la habari la Sudan Suna linaripoti kwamba mkuu huyo wa jeshi amekutana na Mfalme Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani mjini Doha, na kujadili masuala ya ushirikiano kati ya nchi zao mbili, maslahi ya pamoja na hali nchini Sudan. Burhan alikwenda Cairo na Juba katika juhudi za kupata uungwaji mkono kuweza kumaliza vita nchini Sudan baada ya juhudi mbali mbali za upatanishi kushindwa kuleta amani. Mapigano yalizuka kati ya jeshi la taifa linalongozwa na Burhan na kikosi cha dharura cha RSF kinacho ongozwa na Mohamed Hamdan Dagalo na kusababisha vifo vya karibu watu elfu tano na kuwalazimisha wengine milioni 4 na laki nane kukimbia makazi yao, kulingana na Umoja wa Mataifa. Habari hii inatokana na vyanzo mbalimbali vya habari #voaswahili #voa #sudan #Qatar #vita #ziara #mfalme #Sheikhtamimbinhamadalthani #cairo #juba - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.