Mmea wa dungusi waanza kufaidi wakaazi wa Laikipia

  • | Citizen TV
    433 views

    Wafugaji katika Kaunti ya Laikipia sasa wanatazamia kubadilisha tishio la mmea wa dungusi kakati kwa kuukausha na kuutumia kama lishe kwa mifugo. Utafiti uliofanywa na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Jomo Kenyatta (JKUAT) kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Florida umewasaidia wakulima kubadilisha magugu hayo na kuwa yenye manufaa kwa mifugo wao.