Mnara wenye umbo la wimbi la bahari uliojengwa kwa kutumia chupa za plastiki wazinduliwa mjini Diani

  • | Citizen TV
    652 views

    Mnara wenye umbo la wimbi la bahari uliojengwa kwa kutumia chupa za plastiki umezinduliwa mjini Diani katika kaunti ya Kwale. Mnara huo uliokarabatiwa kwa kutumia Zaidi ya chupa 7,000 unalenga kutoa hamasisho kwa wakaazi na watalii dhidi ya kuchafua mazingira kwa kutupa plastiki ovyo. Hamasisho inaendelezwa na shirika la kijamii la HERI Kenya, halmashauri ya Mazingira nchini NEMA na Serikali ya kaunti ya Kwale.