Moja ya maajabu saba ya dunia: Maajabu ya Victoria Falls

  • | VOA Swahili
    278 views
    Maporomoko ya Victoria Falls, maarufu kama Mosi-oa-Tunya, au Moshi unao Nguruma, ni moja kati ya Maajabu Saba ya Dunia. Eneo la UNESCO la Turathi ya Dunia, maji yake yanatiririka kutoka Mto Zambezi huko kusini mwa Afrika. Ikiwa iko katika mpaka kati ya Zimbabwe na Zambia, maporomoko haya yanachukuliwa ni makubwa kabisa duniani, yenye upana wa mita 1,708 (futi 5,604). Ikiwa ni ushahidi wa jina lake, Mosi-oa-Tunya, maporomoko haya yanaonyesha “moshi” unatokana na ukungu wa mngurumo wa maporomoko ya maji, yakionekana kutoka umbali wa maili kadhaa. Ikiwa na makorongo sita ya asili, maporomoko hayo yanaweza kuonekana katika eneo la Victoria Falls, Zimbabwe na Livingstone, Zambia. #victoriafalls #zimbabwe #livingstone #zambia #voa #voaswahili #mosioatunya #unesco #reels #turathi - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.