- 122 viewsDuration: 2:01Ni afueni kwa wanafunzi elfu nne eneo bunge la Taveta kaunti ya Taita Taveta baada ya hazina ya ustawishaji eneo bunge hilo kuanza kutekeleza mpango wa elimu Bora ambapo wanafunzi wa shule upili za kutwa watasoma bila malipo yoyote.. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mpango huo mbunge wa Taveta John Bwire anasema mpango huo pia unalenga wanafunzi wa shule za mabweni ambapo watalipa shilingi elfu tano kwa mwaka huku fedha zilizosalia zikilipwa na hazina ya NG-CDF.