Mradi wa kisima na usambazaji wa maji wakamilika Garbatula

  • | Citizen TV
    270 views

    Wakazi wa vijiji vya Gafarsa na Iresaboru katika Kaunti Ndogo ya Garbatula, Kaunti ya Isiolo sasa wana kila sababu ya kutabasamu, baada ya kukamilika na kufunguliwa rasmi kwa mradi wa kisima cha maji na usambazaji wa maji safi kwa matumizi ya nyumbani, pamoja na bwawa maalum na birika la kunyweshea mifugo.