Gavana wa kaunti ya Kirinyaga Anne Waiguru ameanzisha mradi wa taa za barabarani katika miji na masoko mbalimbali ili kuchochea uchumi wa saa ishirini na nne, ambapo zaidi ya taa 165 zimewekwa katika maeneo mbalimbali katika kaunti hiyo.
Mradi huo uliotekelezwa na idara ya barabara, uchukuzi na makazi unalenga kuboresha usalama, kuongeza muda wa biashara na kuinua kipato cha wafanyabiashara, huku maafisa wa kaunti wakisema kuwa hatua hiyo imewezesha wafanyabiashara kufanya kazi hadi usiku wa manane na hata saa zote, na wakazi wakiripoti kupungua kwa uhalifu, kuongezeka kwa wateja na mazingira bora ya kibiashara kutokana na mwanga huo.