Skip to main content
Skip to main content

Mshukiwa wa ujambazi Chaiiwali auawa kwa kupigwa risasi Matungulu

  • | Citizen TV
    22,403 views
    Duration: 1:49
    Polisi katika eneo la Matungulu wamempiga risasi na kumuua mshukiwa anayehusishwa na wizi wa kutumia silaha uliotokea katika mkahawa wa Chaiiwali ulioko kwenye Barabara ya General Mathenge, Westlands. Kwa ushirikiano na makachero wa upelelezi, maafisa hao walimfumania mshukiwa huyo katika eneo la Joska, linalodaiwa kuwa maficho yake baada ya kutekeleza ujambazi jijini Nairobi. OCPD wa Matungulu, Peter Gichohi, amethibitisha kisa hicho akisema mshukiwa, Vincent Ochieng, alipatikana akiwa na bunduki moja na risasi sita, mbili zikiwa zimetumika. Kwa mujibu wa majirani, Ochieng alikuwa ameishi eneo hilo kwa muda mrefu na hakuna aliyedhani kuwa ni jambazi kutokana na uhusiano wake mzuri na wakazi. Polisi wanaendelea kuwasaka washukiwa wengine, huku mwili wa Ochieng ukipelekwa katika hifadhi ya maiti ya Hospitali ya Kangundo Level 4.