Mtanzania aliyekufa Ukraine alifungwa na baadaye kujiunga na Wagner

  • | BBC Swahili
    2,758 views
    Mtanzania aliyeuawa nchini Ukraine alikuwa amefungwa jela kwa uhalifu na baadae kujiunga na kundi la Urusi la Wagner akiwa kifungoni. Kwa mijibu wa Waziri wa mambo ya nje ya Tanzania Bw Tarimo aliahidiwa pesa na uhuru wake mara baada ya kukubali kujiunga kisha kupigana vita huko Ukraine. Kwa mujibu wa Waziri Stergomena Tax, mtanzania huyo alikwenda nchini Urusi mwaka 2020 kwa ajili ya masomo ya shahada ya uzamili katika fani ya biashara, lakini mwezi machi 2022 alipatikana na hatia ya uhalifu na kuhudukumiwa kifungo cha miaka 7. Ingawa Waziri huyo hakuweka wazi ni uhalifu gani huo lakini wakati akitumikia kifungo hicho alihaidiwa pesa na uhuru ili akatumikie Urusi vitani huko Ukriane. #bbcswahili #tanzania #uhalifu