Mtoto wa miezi minne apotea katika njia tatanishi hospitalini Kapsabet

  • | Citizen TV
    1,131 views

    Familia moja kutoka eneo la Mosop pamoja na wanaharakati wa haki kaunti ya Nandi wamejitokeza kulalamikia usalama katika baadhi ya hospitali za umma kaunti hiyo.Hii ni baada ya mtoto wa siku nne kupotea katika hali ya kutatanisha. Inaarifiwa kuwa mamake mtoto huyo, alifika katika hospitali ya rufaa ya Kapsabet kujifungua lakini alipokuwa akitayarishwa kurudi nyumbani baada ya kujifungua, hakumuona tena mwanawe.