Skip to main content
Skip to main content

Mudavadi ahimiza pembe ya Afrika kuendeleza amani

  • | Citizen TV
    340 views
    Duration: 2:06
    Mkuu wa waziri Musalia Mudavadi amehimiza nchi za kanda ya pembe ya Afrika, kuongoza juhudi za kutafuta amani bila kutegemea mataifa ya nje, kufadhili shughuli za amani na kuhakikisha makubaliano yanayofikiwa yanatekelezwa kikamilifu ili kuzuia vita. Akizungumza wakati wa maadhimisho ya 40 ya halmashauri ya maendeleo kati ya mataifa , IGAD, jijini Nairobi, amesisitiza haja ya kuimarisha amani na usalama katika pembe ya Afrika . Aidha, Mudavadi ametaja migogoro ya muda mrefu kuwa changamoto kuu na kizingiti cha amani na usalama wa kudumu katika ukanda huu.