Mudavadi ahudhuria mkutano wa mawaziri wa kamati ya muungano wa Afrika mjini Algiers

  • | Citizen TV
    187 views

    Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi, ambaye pia ni waziri wa masuala ya kigeni anahudhuria kongamano la kumi na moja la mawaziri wa kamati ya muungano wa afrika mjini Algiers, nchini Algeria. kamati hiyo ina jukumu la kushinikiza mabadiliko kwenye baraza la umoja wa mataifa kuhusu usalama -UNSC- Ikiwemo uwakilishi wa Afrika kwenye baraza hilo.Mudavadi atahudhuria mkutano wa mawaziri baadaye hii leo mjini Algiers. baadhi ya mataifa wanachama wa kamati hiyo ni pamoja na Uganda, Namibia, Sierra Leone, Libya, Equatorial Guinea, Senegal, Zambia, DRC na Algeria. wiki iliyopita, mudavadi alizindua kamati ya pamoja ya kuendesha kampeni ya kumpigia debe raila odinga kuwa mwenyekiti wa tume ya muungano wa afrika AUC.