Muonekano wa mtaani katika ujirani wa Al Karama unaonyesha uharibifu wa shambulizi la Israel

  • | VOA Swahili
    315 views
    Wakazi wa ujirani wa Al Karama huko Gaza wanarejea kuangalia nyumba zao saa 12 baada ya kukimbia shambulizi holela la mabomu la kushitukiza kwenye majengo yao. Saa chache awali, walipokea ujumbe wa SMS ukiwataka kuondoka na kutorejea kamwe katika makazi yao huku eneo lote likifanywa kuwa ni eneo la kivita lililofungwa. Kanda hii ya video ya VOA inaonyesha muonekano wa eneo la mtaani ambapo wakazi wake wanaondoa vifusi kilichofunika magari, majengo ya makazi na maduka baada ya uharibifu uliosababishwa na mashambulizi ya Israeli. #israel #palestine #gaza #reels #igreels #videography #voa #hamas #gazacity