- 2,861 viewsWaziri wa Usalama, Kipchumba Murkomen, amesema kuwa maafisa wa usalama wanachunguza kisa cha kuchomwa moto kwa mwanamke aliyechora picha ya Rais William Ruto begani mtaani Kasarani. Murkomen pamoja na Inspekta Jenerali wa Polisi, Douglas Kanja, walimtembelea mwathiriwa Rachael Wandeto, ambaye amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kenyatta akiwa na majeraha makubwa. Inaarifiwa kuwa Rachael alishambuliwa na watu waliokuwa kwenye pikipiki alipokuwa akitoka dukani.