Skip to main content
Skip to main content

Murkomen atetea polisi kuitisha pesa za mafuta

  • | Citizen TV
    2,230 views
    Duration: 2:35
    Waziri wa usalama Kipchumba Murkomen amewafokea wanaozua maswali kuhusu kauli yake kwamba maafisa wa polisi wana haki ya kuwaitisha raia mafuta ya magari yao wanapohitajika kutoa huduma za usalama. Murkomen ambaye ameendelea kuwatetea polisi ametaja kama ujinga kusema kuwa tabia hiyo ya polisi ni ufisadi. Aidha Murkomen amesema kuwa wakati mwingi mafuta huwaishia polisi na kuwalazimisha kuomba usaidizi. Na kama anavyoarifu Ben Kirui, Murkomen amesema kuwa wizara yake inazungumza na hazina ya kitaifa kuongeza mgao wa mafuta kwa polisi.