- 499 viewsWaziri wa Usalama wa ndani, Kipchumba Murkomen ametangaza kuanza kwa operesheni ya kiusalama chini ya saa 48 Laikipia Kaskazini. Wakazi wanasema silaha zao zilichukuliwa katika oparesheni zilizopita huku majangili wakiendelea kusalia na silaha zao, jambo lililosababisha mashambulizi mengi yanayoshuhudiwa. Hata hivyo, wengi wanasema si mara ya kwanza kwa ahadi kama hii kutolewa, wakisubiri kuona iwapo itafaulu safari hii