Mvutano wa SautiSol na Azimio

  • | K24 Video
    92 views

    Chama cha hakimiliki ya muziki nchini MCSK kimetetea muungano wa Azimio la Umoja One Kenya kutokana na tuhuma za kutumia wimbo wa wanabendi sauti sol kinyume na sheria za hakimiliki. Kulingana na Mutua, MCSK haikukiuka sheria ya kutoa leseni kwa muungano wa Azimio ambao ulilipa ada ya kucheza nyimbo mbalimbali katika kampeini zao. Afisa mkuu mtendaji wa MCSK sasa ametaka wahusika wa Sautisol wafike kwa chama kuwasilisha malalamiko.