Mvutano wazuka kuhusu ofisi ya Mkuu wa Mawaziri

  • | Citizen TV
    807 views

    Afisi ya mkuu wa mawaziri na waziri wa masula ya kigeni Musalia Mudavadi imepuuza taarifa kutoka kwa mkuu wa utumishi wa umma Felix Koskei kuhusu sehemu inayopaswa kuwa afisi yake. Mudavadi akipuuza agizo linalotaka afisi yake kuwa katika jumba la Old Treasury na kushikilia kuwa ofisi hiyo itasalia katika jumba la Railways. Hii ni kufuatia ripoti za mvutano huu, baada ya taarifa hiyo kutangaza kuwa ofisi ya Railways inafaa kuwa ya waziri wa huduma za umma Moses Kuria ambaye naye amepuuza kuwepo kwa tofauti zozote kati na Mudavadi.