- 3,478 viewsMwanafunzi mmoja kati ya wanne waliolazwa katika Hospitali ya Kenyatta jijini Nairobi na kuruhusiwa kurejea nyumbani ameeleza kuwa washukiwa waliowasha moto katika bweni la Shule ya Upili ya Wasichana ya Utumishi walikuwa na mzozo na walimu. Wakati huohuo, familia ya Faith Koskei , mzazi aliyefariki katika ajali akielekea shuleni kumjulia mwanawe usiku wa mkasa , sasa inakabiliwa na mzigo wa kugharamia mazishi na matibabu.