Mwanafunzi Bungoma atengeneza kreni

  • | Citizen TV
    3,392 views

    Mwanafunzi mmoja katika kaunti ya Bungoma aliyejizolea alama ya 410 kwenye mtihani wa KCPE amewasisimua walimu na familia yake kwa ubunifu wake. Ethan Simiyu ambaye ana ndoto ya kuwa mhandisi ametengeneza kreni. Kwa mujibu wa wazazi wake, Ethan amekuwa akitengeneza vifaa kwa kutumia mitandao kunoa makali yake. Ethan anasema matumizi ya mtandao yalimpa msukumo wa kuwa mbunifu. Mwalimu mkuu wa shule alikokuwa akisomea ethan anasema kuwa mwanafunzi huyo ni miongoni mwa waliofanya vema zaidi kwenye mtihani wa KCPE.