Mwanaharakati na mtaalamu wa mitandao Rose Njeri ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000

  • | Citizen TV
    2,181 views

    Mwanaharakati na mtaalamu wa mitandao Rose Njeri ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi laki moja. Njeri hakusomewa mashtaka baada ya mawakili wake, wakiongozwa na jaji mkuu mstaafu David Maraga, kusema kuwa tuhuma dhidi yake hazikuwa na msingi wowote wa kisheria. Njeri anatuhumiwa kwa kubuni jukwaa la mtandao la kuwasilisha maoni ya umma kuhusu mswada wa fedha wa mwaka 2025.