Mwanamke afariki maji eneo la Gakungu Kirinyaga

  • | Citizen TV
    2,402 views

    Mtu mmoja ameaga dunia na mamia kusalia bila makao kufuatia mafuriko yanayoendelea sehemu mbalimbali nchini. Mwanamke wa miaka sitini na miwili alikufa maji baada ya kuzidiwa na mafuriko alipokuwa akivuka mto Thiba kaunti ya kirinyaga. Haya yanajiri huku waathiriwa wa mafuriko ambao wameachwa bila makao sasa wakiirai serikali kuweka mikakati ya kudumu ili kuzuia mafuriko ya mara kwa mara.