Akiwa na umri wa miaka 17 pekee, Mariam Ibrahim Ndung’u tayari ametambulika katika viwango mbalimbali vya mchezo wa ulengaji shabaha, ambapo amejizolea medali nyingi na kujizolea sifa kama mmoja wa wanamichezo chipukizi wenye mafanikio makubwa.
Mariam Ibrahim Ndung'u ameeleza kuwa mafanikio yake yamekuwa chachu ya kuwahamasisha wasichana na wavulana wengi kujiunga na mchezo huo. Ujasiri wake umeendelea kuonekana kama mfano wa kuigwa katika kukuza vipaji vya vijana nchini.
Mwanahabari Mwanahamisi Hamadi alikutana na Mariam akiwa katika mazoezi huko Bamburi, Mombasa na kuandaa makala maalum ya “mwanamke bomba” kuhusu safari yake ya michezo na mafanikio yake.