Mwanasheria Mkuu Justin Muturi ataka DCI kuwachukulia hatua wazalishaji wa kibinafsi wa umeme

  • | Citizen TV
    919 views

    Mwanasheria Mkuu Justin Muturi ameitaka idara ya upelelezi wa Jinai kuwachukulia hatua wazalishaji wa kibinafsi wa umeme ambao hawajatangaza majina ya wanaofaidika. Akizungumza katika kikao cha kamati ya bunge kuhusu kawi, Muturi amesema wafanyibiashara hao wanavunja sheria na kuwa hakuhusishwa kwenye uamuzi huo ambao umefanya gharama ya umeme kupanda zaidi.