Mwenyekiti wa Royal Media Services na mwenye hisa mkuu wa kampuni ya bima ya Directline Daktari S.K. Macharia ameteua maafisa wapya watakaosimamia oparesheni katika kampuni ya Directline.
Akizungumza alipochukua uongozi wa kampuni hiyo katika makao makuu jumba la Anniversary Towers, Daktari S.K. Macharia aliwatwika majukumu Wilson Wambugu Maina akiwa ndiye kaimu afisa mkuu, Directline, Stella Kinoti atahudumu kama mkuu wa masuala ya fedha, Elizabeth Kuria atakuwa msaidizi wa Kinoti huku James Mari akiteuliwa kuwa meneja wa masuala ya teknolojia. Daktari Macharia amemsimamisha kazi aliyekuwa afisa mkuu wa Directline Sammy Kanyi na kusema mabadiliko aliyoyafanya yanaanza kutekelezwa mara moja.