Mwili wa aliyekuwa afisa wa Hazina Kuu Tom Osinde aliyetoweka hatimaye wapatikana

  • | KBC Video
    77 views

    Harakati za kumtafuta Tom Osinde ziliishia kwa majonzi baada ya familia yake kuutambua mwili wake katika chumba cha kuhifadhi maiti cha hospitali ya kaunti ya Migori. Mwili wa mfanyikazi huyo wa zamani wa wizara ya fedha ulipatikana ukiwa umetupwa katika mto KUJA katika kaunti ya Migori alhamisi iliyopita, wiki tatu baada yake kuripotiwa kutoweka. Maafisa wa polisi hawakujua kuwa mwili huo uliokuwa umeharibika ulikuwa wa Osinde. Familia yake iliutambua mwili huo leo asubuhi na kufikisha kikomo harakati za kumtafuta.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channell: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #Tomoside #darubini