Skip to main content
Skip to main content

Mwizi amtumia paka kuiba

  • | BBC Swahili
    21,439 views
    Duration: 1:24
    Mwanaume mmoja anadaiwa kujaribu kupora benki huko Maryland akitumia paka mdogo ambaye anashutumiwa kumuiba dakika chache tu kabla ya tukio hilo. Magnolia, paka mdogo mwenye rangi nyeusi na nyeupe, alichukuliwa kutoka duka la wanyama la eneo hilo na mwanaume ambaye utambulisho wake haujatangazwa na polisi. Kulingana na mamlaka, mtuhumiwa alikimbia kutoka dukani kuelekea Benki ya PNC iliyo karibu, ambapo anadaiwa kutumia paka huyo kama sehemu ya jaribio lake la uporaji. Na kama anavyoripoti Leila Mohammed @mrs.tadicha Paka huyo kwa jina - Magnolia alipatikana akiwa salama na kwa sasa anapatikana na anatarajiwa kurejeshwa kwa mmiliki wake. - - #bbcswahili #paka #wizi Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw