Skip to main content
Skip to main content

Naibu Gavana akosoa kuchelewa kwa mgao wa elimu nchini

  • | Citizen TV
    246 views
    Duration: 1:14
    Naibu Gavana wa Machakos, Francis Mwangangi, amelaumu serikali kuu kwa kile anasema ni kuzorotesha sekta ya elimu. Akizungumza katika wadi ya Kalama, Mwangangi ameituhumu serikali ya Kenya Kwanza kwa kuelekeza rasilimali zilizokusudiwa elimu kwenda kwenye masuala ya kisiasa. Aidha ameonya kuwa ucheleweshaji wa mgao wa fedha umeathiri shule nyingi, huku baadhi ya taasisi zikilazimika kufunga mapema.