Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat ameondoka mamlakani

  • | Citizen TV
    4,843 views

    Naibu Inspekta Jenerali wa Polisi Eliud Lagat amejiondoa mamlakani kwa muda kutoa nafasi ya uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanablogu Albert Ojwang. Kwenye taarifa, Lagat amesema amechukua hatua hiyo ili kuipa ipoa nafasi ya uchunguzi bila ushawishi wowote. Hatua hii pia inafuatia msururu wa shinikizo za kumtaka aondoke ofisini.