Naibu Rais Gachagua afungua rasmi maonyesho ya kilimo na biashara katika kaunti ya Mombasa

  • | K24 Video
    46 views

    Serikali imesema mikakati iliyoweka ya kuimarisha uchumi na kupunguza gharama ya maisha imeanza kuwa na ufanisi. Akiongea katika maonyesho ya kilimo na biashara katika kaunti ya Mombasa naibu rais Rigathi Gachagua amesema kuwa mbolea iliyotoa kwa wakulima imechochea kupatikana kwa mazao tele na hivyo bei za bidhaa za msingi imepungua.