Naibu rais Gachagua awataka wakazi wa mlima Kenya wasikubali kugawanywa kisiasa

  • | K24 Video
    101 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua na baadhi ya wanasiasa kutoka eneo la Mlima Kenya wamekashifu hatua ya kuidhinishwa kwa mbunge wa kiharu ndindi nyoro kuwa mgombea mwenza wa Rais William Ruto kutika uchaguzi ujao wa 2027. Kulingana na viongozi hao, ni mapema mno kuanza siasa zinazotishia umoja wa Mlima Kenya na kuwa nia ya kuugawanya mlima hautafaulu kamwe.