Naibu rais Kithure Kindiki aongoza msafara wa Kenya Kwanza huko Kilifi

  • | Citizen TV
    1,014 views

    Naibu Rais Kithure Kindiki amempigia debe Rais William Ruto kuhudumu kwa mihula yote miwili akisema serikali ya Kenya Kwanza inalenga kutimiza manifesto yake badala ya kujihusisha na siasa potovu. Akizungumza katika kaunti ya kilifi kwenye hafla za kupiga jeki makundi ya kina mama na vijana katika kaunti hiyo, Kindiki na viongozi alioandamana nao amesema taifa halina nafasi ya migawanyiko ya kikabila. Viongozi hao wamesuta upinzani wakisema ni viongozi wasio na agenda ya kuwaleta pamoja wakenya.