- 112 viewsKenya imejizatiti kuongeza rasilimali kwa wanawake wanaohusika katika kampeni za amani, usalama na mabadiliko ya hali ya tabianchi. Akiongea katika hafla iliyokuwa jijini Nairobi wikendi, mwakilishi wa kudumu wa Kenya kwa UN-Habitat, Susan Nakhumicha alibaini kuwa wanawake wa tabaka la chini wameathiriwa mno na hali mbaya ya hewa na hivyo wanahitaji msaada.