NCIC yaendelea kuhamasisha viongozi kuhusu umuhimu wa amani na utangamano

  • | K24 Video
    110 views

    Huku tume huru ya uchaguzi na uratibu wa mipaka nchini ikiendelea kuwaidhinisha wawaniaji mbalimbali, tume ya mshikamano wa kitaifa, NCIC inaendelea kuhamasisha viongozi kuhusu umuhimu wa amani na utangamano. Katika kaunti ya Bungoma, NCIC iliandaa warsha ya kuhamasisha viongozi wa sekta tofauti kuhusu umuhimo wa kuwa na kampeini za amani.