Skip to main content
Skip to main content

Ndindi Nyoro apendekeza kupunguza gharama za serikali kushusha bei ya mafuta

  • | Citizen TV
    507 views
    Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro amependekeza kupunguzwa kwa gharama za safari za serikali za ng’ambo kwa shilingi bilioni 100, akisema pesa hizo zinafaa kutumika kupunguza bei ya mafuta nchini kwa shilingi 17 kwa diseli na shilingi 15 kwa petroli. Akiwasilisha pendekezo lake mbele ya Kamati ya Bunge la Taifa kuhusu bajeti, mbunge huyo vilevile amekosoa mpango wa G2G wa serikali wa kuagiza mafuta moja kwa moja, akisema hauwezi kudhibiti bei ya juu ya mafuta.