- 578 viewsDuration: 2:04Mbunge wa Kiharu Ndindi Nyoro ameishinikiza serikali kufanya masomo kuwa ya bure, akisema kuwa inawezekana. kauli ya nyoro inajiri baada ya wizara ya elimu kukiri kuwa gharama ya elimu ya bure ya sekondari haijulikani. Nyoro amesema kuwa serikali inaweza kufanya elimu kuwa ya bure kwa kuongeza uadhili wa wanafunzi wa sekondari kutoka shilingi 22,000 kwa kila mwanafunzi hadi shilingi 31,000. Nyoro amesema kuwa serikali itahitaji kutenga shilingi bilioni 30 pekee kuafikia hayo.