Skip to main content
Skip to main content

Nduta Mbogori: 'Baada ya kuthibitishwa kuwa nina Parkinson nilitamani kufa'

  • | BBC Swahili
    3,572 views
    Duration: 7:14
    Nduta Mbogori, mwenye umri wa miaka 34, anaishi na ugonjwa wa Parkinson, ambao huathiri mfumo wa neva. Anasema ugonjwa huu hauanzi ghafla, bali hujitokeza taratibu hadi kufikia hatua ya kutambuliwa. Anapotafakari maisha yake ya nyuma, Nduta anaamini dalili za ugonjwa huo zilianza tangu akiwa mtoto, ingawa yeye na familia yake hawakuwa na ufahamu wa kile alichokuwa akipitia wakati huo. Nduta ndiye Waridi wa BBC wiki hii. Katika simulizi yake, anasimulia safari yake ya maisha, changamoto alizokumbana nazo akiwa na Parkinson, na nguvu zinazomwezesha kuendelea kusonga mbele licha ya ugonjwa huo. Mwandishi: Asha Juma #bbcswahili #waridiwabbc #kenya Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw