'Nilijipaka damu ya waliouawa kichwani, masikioni na mdomoni hivyo ndivyo nilivyonusurika'

  • | BBC Swahili
    804 views
    Mmoja wa wanafunzi aliyenusurika na mashuhuda wa shambulizi katika shule lililotokea siku ya Ijumaa huko Uganda wanaelezea tukio hilo la kusikitisha lililoua watu takriban 40 lilivyotokea. Wengi wa waathiriwa walikuwa wanafunzi wa shule ya Lhubiria iliyoko katika mji wa Magharibi wa Mpondwe. Kundi la Wanamgambo wenye uhusiano na Islamic State Allied Democratic Forces (ADF) wamelaumiwa kwa shambulio hilo. #bbcswahili #uganda #waasi