Nimewasamehe madereva walioniacha nikaliwa na fisi porini

  • | BBC Swahili
    1,827 views
    Irene Mbithe mwenye umri wa miaka 27 ni mtoto wa kwanza kati ya watoto sita katika familia yake kutoka machakos. Irene ni mmoja wa wale ambao maisha yao yalivurugika alipovamiwa na fisi, anasimulia jinsi alivyopoteza mkono wake, na jicho katika shambulio baya baada ya madereva wa lori kumshukisha njiani usiku wa manane katika hifadhi ya mbuga ya wanyama alipokataa wamnyanyase kingono. Hapa ndipo Irene Mbithe alipokutana ana kwa ana na fisi aliyemshambulia vibaya, kwa kumtafuna uso upande wa kushoto na kumsababishia ulemavu wa jicho moja ambalo mpaka sasa halioni. Amemsimulia Hamida Abubakar katika waridi wa BBC #bbcswahili #kenya #waridiwabbc Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw