11,601 views
Duration: 9:11
Chama cha ACT Wazalendo kinasubiri majibu kutoka serikalini kuwasilishwa mahakamani hapo tarehe 3 Septemba. Chama hicho kilikwenda Mahakama Kuu ya Tanzania, Masijala Kuu Dodoma kufungua kesi dhidi ya Tume ya Uchaguzi na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kupinga uamuzi wa Tume wa kumuengua mgomba wake wa urais Luhaga Mpina kwa madai kwamba uteuzi wake ulikiuka Katiba, Sheria na Kanuni za chama hicho.
Madai haya yalitoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Kwenda Tume ya Uchaguzi. Sasa kupata ufafanuzi wa kisheria kuhusu pingamizi hili dhidi ya Mpina, mwenzangu Sammy Awami amezungumza na mwanasheria Fulgence Massawe, ambaye miaka sita iliyopita ofisi yake na wadau wengine wa siasa walifungua kesi Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki kupinga mamlaka mapana ya ofisi ya Msajili wa Vyama.
Sammy alianza kwa kumuuliza Massawe ikiwa ameshangazwa na mlolongo wa matukio na maamuzi yaliyopelekea kuenguliwa kwa Mpina
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw