Norway: Mwanaharakati aliyeko kifungoni Iran Narges Mohammadi ashinda Tuzo ya Amani ya Nobeli

  • | VOA Swahili
    167 views
    Mwanaharakati raia wa Iran anayetetea haki za wanawake aliyefungwa gerezani Narges Mohammadi, ameshinda Tuzo ya Amani ya Nobel Ijumaa ikiwa ni kama kuukemea uongozi wa kibabe na kuweka nguvu dhidi wa waandamanaji wanaoipinga serikali. Kamati inayoandaa tuzo hiyo imesema ni kuwapa heshima wote wale walioongoza maandamano ya hivi karibuni ambayo hayajawahi kushuhudiwa nchini Iran na kutaka kuachiliwa kwa Mohammadi mwenye umri wa miaka 51 ambaye alifanya kampeni kwa miongo mitatu ya haki za wanawake na kupinga hukumu ya kifo. “ tuna tumaini ya kupeleka ujumbe kwa wanawake kote duniani ambao wanaishi katika mazingira ambayo wanabaguliwa; kuweni na ujasiri, endeleeni, Berit Reiss- Andersen mkuu wa kamati ya tuzo ya Nobel ya Norway ameliambia shirika la habari la ROITA. Hakukuwa na majibu rasmi kutoka Tehran ambayo inaita maandamano hayo kuwa nu uasi unaoongozwa na magharibi. Mohammadi anatumikia vifungo mbali mbali katika gereza la Evin mjini Tehran takriban miaka 12 jela moja ya vipindi vingi ambavyo amekuwa akizuiliwa gerezani , hiyo ni kulingana na shirika la kutetea haki za watetezi walio mstari wa mbele. #mwanaharakati #haki #wanawake #uhuru #tuzoyaamaninobel #NargesMohammadi #irani #voa #voaswahili - - - - - #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.