- 144 viewsRipoti ya Tume ya Maadili na kupambana na ufisadi ya mwaka wa 2024-2025 imeonyesha kuwa rushwa ilibaki kuwa kosa lililoripotiwa zaidi nchini. Masuala ya ufujaji wa fedha, mwenendo usio wa kimaadili na ununuzi wenye udanganyifu yaliorodheshwa kama masuala yaliyoripotiwa na kuchunguzwa na tume. EACC pia imesikitishwa na kuongezeka kwa idadi ya maafisa wa serikali na umma ambao hutumia vyeti bandia za kitaaluma kupata ajira.