Orindo aliyepata alama 374 KCPE arejea Gredi ya 6 kwa kukosa karo ya kujiunga na kidato cha kwanza

  • | KBC Video
    105 views

    Mwanafunzi aliyepata alama 374 katika mtihani wa kitaifa wa KCPE mwaka jana amewashangaza wengi katika eneo la Kakuro kaunti ya Kisumu baada ya kuamua kurejea Gredi ya 6 katika shule yake ya zamani. Jerry Orindo anasema aliamua kurejea katika shule yake ya msingi ya zamani ya St. Mercy baada ya kukosa kupata karo kumwezesha kujiunga na shule ya upili. Aidha mtahiniwa mwingine alilazimika kutembea umbali wa kilomita 600 kutoka kambi ya wakimbizi ya Kakuma eneo la Turkana hadi shule ya upili ya Kabianga huko Kericho kujiunga na kidato cha kwanza bila karo na mahitaji mengine ya shule.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive