Owalo asema mtandao wa Tiktok unatoa nafasi za ajira kwa vijana

  • | KBC Video
    43 views

    Waziri wa habari, mawasiliano na uchumi dijitali Eliud Owalo sasa analitaka bunge kuudhibiti mtandao wa kijamii wa TikTok badala ya kuupiga marufuku. Akiongea alipofika mbele ya kamati ya bunge kuhusu malalamishi, Owalo alisema kupiga marufuku mtandao huo kutawanyima mamilioni ya vijana mapato ya kila siku na kusababisha kuondoka kwa wawekezaji wengi kutoka sekta ya kibinafsi wanaohudumu kupitia mfumo wa dijitali. Baadhi ya wabunge hata hivyo wana wasiwasi iwapo serikali ina uwezo wa kudhibiti maudhui kabla ya kuchapishwa kwenye mtandao huo wa TikTok.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive