Polisi jijini Nairobi wawatawanya waandamanaji Kaloleni

  • | Citizen TV
    2,683 views

    Polisi jijini Nairobi waliwatawanya waandamanaji kutoka ukumbi wa kijamii wa Kaloleni kuelekea Bunge la kitaifa waliopinga mswada wa fedha wa mwaka wa 2024. Kundi hili linalojitiita The concerned Citizens Kenya na Linda Jamii wakiongozwa na viongozi wao Joseph Mugachia na wakili Fred ogola walitawanyishwa kabla ya kufika kwenye majengo ya bunge walimokuwa wakielekea ili kulalamikia mswada wa kifedha wa mwaka 2024/2025 na ushuru unaotozwa wakenya.