- 20,231 viewsDuration: 2:42Polisi wa eneo la Kilimani jijini Nairobi wanachunguza kisa ambacho msichana mwenye umri wa miaka 21 amefariki baada ya kuanguka kutoka kwenye jengo moja jijini Nairobi. Margaret Wambui alianguka kwa njia tata kutoka kwenye jumba hilo la ghorofa 22. Familia yake sasa inadai haki na ripoti ya nini hasa kilichojiri kabla ya kuanguka kwake kutoka ghorofani, kama Gatete Njoroge anavyotuarifu.