- 1,210 viewsDuration: 1:29Polisi mjini Nyeri wanamsaka mshukiwa mmoja wa utengezaji wa pombe ghushi, baada ya kupata kiwanda cha pombe kisicho na leseni ndani ya boma moja eneo la Classic viungani mwa mji wa Nyeri. Kwenye operesheni hiyo, lita mia mbili sitini za ethanol zimenaswa, huku mihuri ya mamlaka ya kukusanya ushuru yenye thamani ya shilingi milioni tano pia ikipatikana. Kulingana na Naibu kamishna Nyeri ya Kati Maina Ngunyi, pombe iliyokuwa ikitengezewa kwenye makazi hayo tayari imefika madukani, na inahusishwa na vifo vya baadhi ya waraibu wa pombe eneo hilo.