Polisi waua jambazi sugu eneo la Makadara huku msichana akiuawa tena mtaani Kasarani, Nairobi

  • | K24 Video
    1,013 views

    Maafisa wa polisi jijini Nairobi katika kituo cha polisi cha Makadara wamemuua mshukiwa sugu wa ujambazi anayesemekana kusababisha matukio ya uhalifu katika maeneo ya Kibra, Langata na Kilimani. Polisi wanadai kuwa mshukiwa huyo wa ujambazi alimpiga risasi mwanafunzi wa sekondari hivi majuzi huko Langata na amekuwa akitafutwa baada ya kisa hicho..