Polisi wawaua washukiwa wawili wa uhalifu katika eneobunge la Githunguri kaunti ya Kiambu

  • | Citizen TV
    655 views

    Washukiwa wawili wa uhalifu wamepigwa risasi na kuuawa katika eneo la Kiriko eneobunge la Githunguri. Wawili hao wanashukiwa kuwa wezi wa vipuri vya magari katika eneo hilo. Kamanda mkuu wa polisi Kiambu Perminus Kiio anasema majambazi wanne walivamia boma moja eneo hilo na kujaribu kuendeleza uhalifu huku wakiwa wamejihami. Wakaazi wa kijiji cha Kiriko wamekuwa wakilalamikia kuhangaishwa na wahalifu eneo hili.