- 4,801 viewsDuration: 4:33Milima ya Eldama Ravine yanatambulika kwa mandhari tulivu na ya kuvutia, lakini katika kijiji cha Poror amani iliyoko imetatizwa na matukio ya kusikitisha. Matumizi ya pombe haramu imesababisha vifo na kuathiri familia nyingi hapa. Brenda Wanga anaangazia masaibu ya kijiji hiki ambacho kimevamiwa na pombe haramu ambayo wakaazi wanasema inauzwa na watu ambao wanapasa kuwasaidia wananchi.